Wadau wa Mtandao wa Ukeketaji watua wilaya za Serengeti na Tarime kutoa elimu
Afnet Dodoma
Published by Thobius Mtui · dpoeonrtSs14chf241m08824tcum6110h9g7tc19868lg9it5tua3u807498 ·
Mtandao wa kutokomeza ukeketaji Tanzania (Tanzania Network to end FGM) wametembelea wilaya ya Serengeti na Sirari ili kutoa elimu kwa jamii hiyo (community engagement) ili kuondokana mila zenye madhara hasa ukeketaji. AFNET pia ni mwanachama wa mtandao huu hapa Tanzania.
Kwa mujibu wa Mwenyekiti wa Mtandao wa Kupinga Ukeketaji Tanzania, Francis Selasini, jamii kuendelea kukumbatia mila potofu kunaathiri nguvu kazi ya jamii na taifa kwa ujumla.

Amesema lengo la wao kufika katika maeneo hayo kutoa elimu ni kuhakikisha jamii inaondokana na mila hizo kwa sababu zimeendelea kuleta madhara mengi kwa jamii.
“Na si tu kuleta madhara lakini kuendelea kukumbatia mila kunachangia kuleta umasikini kwenye kaya na jamii na taifa kwa ujumla na mbali na hivyo pia inatusababishia gharama zisizo na sababu,”amesema Selasini.